Ili kuelewa msukosuko huu, lazima turudi mwanzo.
CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo) ilianzishwa rasmi mwaka 1992 wakati Tanzania ilipokuwa ikibadilisha mfumo wa vyama vingi. Waanzilishi walikuwa mchanganyiko wa wanasiasa, wanaharakati, na watu wa sekta binafsi waliotaka mfumo wa kisiasa unaoweka msisitizo kwa uwajibikaji na uhuru wa kiuchumi. Miongoni mwa watu waliotajwa katika historia ya chama kuna majina ya viongozi wa sekta mbalimbali, akiwemo Edwin Mtei, mwanasheria mashuhuri Bob Makani na wengine wengi. Hawa hawakuwa wanamapinduzi, walikuwa wanakapitalisti waliochoshwa na uendeshaji wa serikali ya wakati huo.
Wafadhili wa awali: wafanyabiashara na sekta binafsi
Katika miaka ya mwanzo, CHADEMA ilivutia msaada wa watu wenye uwezo na wafanyabiashara waliotaka sera zinazorahisisha biashara na uwekezaji. Michango hiyo mara nyingi haikuonekana hadharani; ilitolewa kwa njia za ndani au kwa msaada wa kimkakati ili kuimarisha miundombinu ya chama na kampeni za kukujenga chama mikoani. Kujiunga kwa viongozi wenye umaarufu kuliongeza mvuto wa chama kwa wafadhili na wafuasi.
CHADEMA ilikua kwa kasi kubwa sana baada ya Edward Lowassa alitangaza kujiunga na mwaka 2014, hatua iliyosababisha gumzo kubwa na kuongeza umaarufu wa chama na kuvunja rekodi kwenye historia ya siasa za vyama vingo. Kujiunga kwake kulionyesha uwezo wa CHADEMA kuvutia viongozi wa ngazi ya juu kutoka upande wa pili wa kisiasa. Mabepari walifungua mikoba yao, wakimimina fedha nyingi kuunga mkono chama.
Hata hivyo, kila kitu kilibadilika baada ya kuingia kwa uongozi mpya wa Tundu Lissu. Uongozi wake na wa viongozi wenzake wa kisiasa uliashiria mabadiliko ya mkazo wa chama kuelekea masuala ya haki za kiraia, uwazi, na masuala ya kijamii. Hii ilileta mabadiliko ya mtazamo wa chama ambayo baadhi ya wafadhili waliona hayakuwa ya kuendeleza maslahi ya kiuchumi.
Athari na changamoto za mabadiliko bila mkakati
Mabadiliko haya ya mwelekeo wa chama yameathiri chanzo cha ufadhili kwa operesheni za CHADEMA kwenye Nyanja kadhaa. Ni wazi CHADEMA imepoteza uaminifu wa wafadhili wa sekta binafsi. Haswa Kundi la wafanyabiashara wanaotaka sera za soko huria wamesita kuendelea kutoa michango baada ya chama kuoonyesha msimamo wa kisoshalisti au kinachokosoa tu sekta binafsi bila kujaribu kuelewa changamoto zao.
Upungufu wa rasilimali za kampeni umeonekana wazi, bila michango kubwa, chama kinakosa uwezo wa kuendesha kampeni za kitaifa, kulipa miundombinu ya chama, na kumudu gharama za kisheria na mahitaji ya wanachama.
Hizi ni baadhi ya atahari za madiliko yaliyotokana na chama kilijikita na wanaharakati ambao wanaamini "wafanyabiashara hawana shida." Mabadiliko ya mwelekeo bila mkakati wa kuunganisha tabaka tofauti za wafuasi (wafanyabiashara, wanaharakati, wanasiasa wa jadi) umeacaha pengo la utekelezaji.
CHADEMA sasa inahitaji sera zinazoonyesha jinsi masuala ya kijamii (kama kupunguza umaskini) yanavyoweza kuendana na sera za kukuza biashara ili kuwashirikisha wafadhili na wafuasi kwa pamoja.
Wafanyabiashara na wawekezaji wanaotazama uongozi huu wanaona chama kinachobeza matatizo yao na kuwafanya kuwa maadui. Kwa nini mfanyabiashara awekeze kwenye chama kinachomtukana?
Bado hakuna maoni yaliyoidhinishwa. Kuwa wa kwanza kuchangia.